Posts

Majuto Ni Mjukuu

 Azizi Ni kipusa aliyezaliwa na kulelewa kwa njia ya kipekee. Binti huyu mwenye maumbile ya kupendeza na sura nzuri alivutia wengi, wa karibu na mbali, kwenye vitongoji hadi vijiji, wazee kwa vijana, bila shaka alikuwa mfano bora wa binadamu aliyeumbwa akaumbika. Pasi na sura, Azizi alikuwa binti mwenye hulka njema, wengi walimsifia kwa heshima aliyokuwa nayo kwa waliomzidi umri, shuleni alipendwa na walimu, kwani kwenye buku hakuachwa nyuma. Alikua miongoni mwa wanafunzi bora na kila muhula alitunukiwa zawadi chungu furika, ama kweli, Chanda chema huvikwa Pete na mcheza kwao hutuzwa. Kadri siku zilivyozidi, Azizi naye maisha yake yalianza kubadilika. Alimaliza shule ya upili na kufuzu kwa alama nzuri tu, hivyo akajipa nafasi ya kujiunga na chuo kikuu. Hapo ndipo maisha yake yalianza kufuata mkondo usioeleweka! Au ndio kitumbua kiliingia mchanga? Na kidagaa kumuozea? Azizi alikuwa si yule Azizi tuliyemjua! Alibadilika na kuwa asiyeambilika wala kusemezeka, hakuskia la mwadhini ...